AWESO AKAGUA UTEKEZAJI WA MRADI WA MAJI WA BANGULO

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amekagua kituo (pampu) cha kusukuma maji Kibamba mkoani Dar es Salaam ambacho ni sehemu ya Mradi wa Maji wa Bangulo unaosanifiwa na kutekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), ikiwa ni sehemu ya ziara yake katika Maadhimisho ya Wiki ya Maji ambayo yatafikia kilele chake Machi 22, 2025 kwa kuadhimishwa kitaifa mkoani Dar es Salaam
Kituo hicho kinasukuma maji mpaka Bangulo Hali ya Hewa kulipojengwa tenki kubwa la kuhifadhi maji la Bangulo la ukubwa wa lita milioni 9 lililopo mtaa wa Bangulo, kata ya Pugu Station wilayani Ilala ambako Aweso ametembelea pia.


Mradi huu unahusisha Manispaa za Ubungo, Temeke, na Jiji la Ilala, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha huduma ya maji katika maeneo yenye changamoto ya upatikanaji wa maji ukilenga kunufaisha wananchi 450000 wa kata wilayani Ilala za Mzinga, Kipunguni, Kitunda, Pugu station na Kiluvya huku kata za Msigani wilayani Ubungo na Kinyerezi wilayani Ilala zikienda kuongezewa msukumo wa maji. Aidha kwa upande wa Ubungo
Kwa mujibu wa taarifa ya Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA mhandisi Mkama Bwire wakati wa ziara ya Waziri Aweso, mradi huu umegharimu jumla ya fedha za Kitanzania Shilingu bilioni 36.8 hii inajumuisha gharama ya ujenzi pamoja na usimamizi wa mradi ambapo kwa ujenzi pekee gharama ni Shilingi bilioni 35.0 na usimamizi wa mradi gharama ni Shilingi bilioni 1.8
Mradi huu umetekelezwa kwa muda wa miezi 12 chini ya usimamizi wa mhandisi mshauri M/S SCET TUNISIE kutoka Tunisia kwa kushirikiana na SMARCON kutoka Tanzania kwa ufadhili wa Benki ya Dunia.


Aidha Mhandisi Mkama amesema mradi huu ni miongoni mwa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025, ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020, inayolenga kuhakikisha kuwa ifikapo mwaka 2025, upatikanaji wa huduma ya maji unafikia asilimia 85 kwa maeneo ya vijijini na asilimia 95 kwa maeneo ya mijini.