SAMIA WA KIZIMKAZI, ANAMPA USINGIZI MZURI JPM WA CHATO

0
samia-hassan-suluhu-tanzanie

Wakati nchi nzima ipo kwenye taharuki baada ya kifo cha Rais wa awamu ya tano, John Pombe Joseph Magufuli, ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwenye historia ya Tanzania Rais kufia madarakani, wingu jeusi lilitanda kwenye ardhi yetu na Mwamba kutoka Chato umelala, ni majira ya saa tano usiku ndio Makamu wake wa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan anautangazia Umma juu ya kifo hiki, korido za Mamlaka, ulingo wa kisiasa na vijiwe vilisubiri nini kitafuata.

Sio serikali ya CCM, sio Wapinzania na sio Watanzania kila mmoja alibaki na maswali kama JPM amelala yale aliyoyaota, kuyaasisi na kuyawaza yatatimia? Mrithi wake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri atayaendeleza? Maswali magumu ambayo yalikuwa na majibu mepesi sana kwenye kichwa cha SSH, Mwanasiasa aliyeandaliwa kuongoza na sio kutawala, Mwanasiasa aliyeandaliwa kuwa na nguvu pamoja na mamlaka bila kutumia nguvu, karama kutoka kwa Mwenyezi Mungu, baada ya Machi 17 ilifuata historia bora ya yeye kuchukua nchi, kuiponya majeraha, kuivusha kama Mussa wa Wanaisrael kuelekea Kanaani.

Hayati JPM aliacha mradi wa treni za Umeme ama SGR kuunganisha Dar Es Salaam na Morogoro ya Afande Sele na Waluguru, Hayati JPM aliacha mradi wa kuunganisha Mashariki mwa Bahari ya Hindi na Dodoma kwa Chief Mazengo, waulize Watanzania ndoto imetimia? Majibu ni NDIO kwa herufi kubwa reli imekamilika na masaa machache yanatosha kula lunch Dodoma kisha chakula cha usiku ule Manzese, Dar Es Salaam, alishika mradi, akaiishi ndoto na sasa wanaishi uhalisia Watanzania.

Waulize tena Watanzania kuhusu mradi wa Umeme wa Mwalimu Nyerere, umefikia wapi? Mradi ambao serikali umetumia zaidi ya Trilion 6.5 za Kitanzania na sasa upo asilimia 99.8 kukamilika na uanze rasmi kufua Umeme, huku mashine nane kati ya tisa zikiingia Megawati 1,880 kwenye gridi ya Taifa, mnaziona dalili, mnaziheshimu ishara na mnapaswa kuchora mstari wa heshima kuwa huyu Mama kutoka Kizimkazi hajaacha kitu, anaishi ndoto za JPM ili Mtangulizi wake aendelee kulala kwa amani huko Chato.

Mwanachato JPM alikuwa na ndoto za Watani zake Wagogo kupanda ndege, alikuwa na dhamira ya kweli ya kulifufua shirika la Anga, kila mmoja ameshuhudia serikali ya Awamu ya sita chini ya SSH namna imeenzi ndoto hii, kwasasa shirika lina ndege zaidi ya 10 kuhakikisha ndoto hii inaendelea kumea na kuchipua, ndie Rais aliyeshikilia dhana nzima ya mwendelezo wa maono yake na Mtangulizi wake, ni nadra Afrika kuwa na aina hii ya Kiongozi, ni nadra Afrika kuwa na Rais mwenye mwendelezo kama SSH.

Bila shaka JPM anapumzika kwa amani, alivyoacha vingi vinaendelezwa sio barabara, sio Madaraja, sio utetezi wa Wanyonge, sio nidhamu ndani ya Chama na serikalini ni jumla wa kila kitu katika kuhakikisha Tanzania moja inalindwa, maendeleo yanasonga na ndoto za Taifa zinatimia, Pumzika kwa amani JPM.

Lala JPM sasa ni Kazi na Utu, Tunasonga mbele.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *