WAZIRI KIJAJI AKUTANA NA WAZIRI WA UVUVI NA UCHUMI WA BULUU WA USHELISHELI

0

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri Kiongozi na Waziri wa Uvuvi na Uchumi wa Buluu wa nchini Ushelisheli Mhe. Jean Ferrari mazungumzo hayo yamefanyika leo tarehe 28.2.2025, jijini Victoria, Ushelisheli.

Aidha Dkt. Kijaji yumo nchini humo kwa lengo la kushiriki Mkutano wa Tatu wa Mawaziri wa Uvuvi wa Nchi za Ukanda wa Kusini Magharibi mwa Bahari ya Hindi unaotarajiwa kufanyika leo Februari 28, 2025.

Mazungumzo hayo ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Ushelisheli katika masuala ya Uvuvi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *