RAIS SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI MKING – HOROHORO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan leo tarehe 27 Feb 2025 ameweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Mradi wa Maji Mkinga – Horohoro ambao unatumia chanzo cha Bwawa la Mabayani.
Ujenzi wa Mradi huu unatokana na changamoto kubwa ya maji kuwa na chumvi katika ukanda wa vijiji vya mwambao wa bahari. Hivyo, Mradi huu una lengo la kuboresha huduma ya majisafi na salama kwa wananchi zaidi ya 57,334 wa kata 10 katika vijiji 37 vilivyopo pembezoni mwa barabara ya Tanga – Horohoro pamoja na wananchi wa eneo la Horohoro Mpakani.

Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi M/S. STC Construction Company Limited ulianza tarehe 5/11/2022 na unatarajia kukamilika tarehe 05/10/2025.
Utekelezaji wa Mradi huu umefikia asilimia 45 ambapo usanifu wa mradi mzima umekamilika na kazi zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Tayari Bomba kubwa za umbali wa km 37 zimeletwa eneo la Mradi, na bomba zenye urefu wa km 25.5 zimelazwa.
Ujenzi wa matanki mawili ya maji yenye mita za ujazo 200 na 250 umekamilika


Ujenzi wa matanki matatu ya maji yenye mita za ujazo 500 umefikia asilimia 95, na
Ujenzi wa matanki matano ya maji yenye mita za ujazo 100 umefikia asilimia 90.
Gharama ya mradi wa maji Mkinga-Horohoro unatekelezwa kwa kutumia fedha za Serikali kupitia Mfuko wa Taifa wa Maji (NWF) na utagharimu jumla ya shilingi 35,472,451,838.59 ambapo mpaka sasa fedha zilizolipwa kwa Mkandarasi ni shilingi 11,320,867,775.79.
Kukamilika kwa mradi huu kutasaidia kuboresha upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama wananchi zaidi ya 57,334 waishio katika vijiji 37 vya Wilaya ya Mkinga ambao kwa sasa wanapata huduma ya maji kutoka mbali na maeneo yao na ambayo si salama.
#UhondoTVUPDATES