RAIS SAMIA AIVUSHA WIZARA YA MAJI KUTOKA KUWA YA LAWAMA NA KUWA WIZARA YA MFANO

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan leo Februari 25, 2025 ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa maji wa miji 28 utaohudumia miji ya Handeni,Korogwe, Muheza na Pangani.

Aidha mheshimiwa Rais amesema “Wizara ya Maji mmetoka kuwa Wizara ya Lawama na kuwa Wizara ya Mfano, nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya”

Mwaka 2021 tulikuwa tunasukumana sana, lakini tangu mwaka 2022 Sekta ya Maji mmekuwa mnafanya vizuri. Kazi yangu ni kutafuta fedha, nyie kazi yenu uteklezaji Nawapongeza watumishi wote wa Sekta ya Maji, endeleeni kuchapa kazi. amesema Rais Samia.

Amesema amefanya kazi kubwa ya kutafuta fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na amekuwa akitiwa moto na wizara kutokana na usimamizi mzuri ambao umewezesha mafanikio makubwa katika usimamizi na utekelezaji wa miradi.

Awali akizungumza mbele ya Rais, Waziri wa Maji Mheshimiwa Jumaa Aweso (Mb) amesema Wizara ya Maji imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na ushirikiano wanaoupata kutoka kwa Rais Samia. Amesema miradi mingi ya maji imeweza kutekelezwa kwa wakati kutokana na utayari wa Rais Samia kuruhusu fedha ya utekelezaji wa miradi hiyo

Rais samia yuko katika ziara ya kikazi mkoani Tanga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *