TANZANIA NA HUNGARY KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA YA MAJI

0


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), ametembelea Wizara ya Nishati ya Hungary na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia pia masuala ya mazingira Bi. Aniko Raisz.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Kombo alieleza kazi kubwa inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi kupikia barani Afrika pamoja na lengo la kuhakikisha asilimia 80 ya shughuli za upishi nchini zinatumia nishati safi ili kupunguza uharibifu wa mazingira.

Vilevile, Mhe. Kombo alibainisha nia ya Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia katika kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanafikiwa na huduma ya nishati ya umeme. Aidha, alieleza kuwa, kutokana na jitihada hizo, Tanzania ilikua mwenyeji wa Mkutano wa Nishati Barani Afrika uliowaleta pamoja Wakuu wa Nchi na Serikali wa Afrika na kuazimia kuunganisha kaya milioni 300 na huduma ya umeme.

Aidha, kwa kutambua uzoefu na uwezo wa Hungary, ilikaribishwa kushirikiana na Tanzania katika sekta ya nishati ikiwemo kuwekeza katika uzalishaji na usambazaji wa nishati hususan umeme wa jua na joto ardhi.

Hungary ina uzoefu mkubwa katika kutibu na kudhibiti taka, hivyo Mhe. Waziri alikaribisha Hungary kuungana na Tanzania katika kutumia teknolojia zake za kisasa za kudhibiti taka na kuwajengea uwezo wa kitaalamu watanzania katika teknolijia hiyo.

Kwa upande wake Bi. Raisz alieleza kuwa Hungary iko tayari kuanzisha programu za kujengeana uwezo na kubadilishana utalaamu katika sekta ya nishati na mazingira ili kuendelea kuifanya dunia kuwa sehemu salama.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *