VIJANA LAZIMA TUYASEME MAKUBWA YANAYOFANYWA NA  DKT. SAMIA – SHAMIRA

0

Mjumbe wa Baraza kuu UVCCM Taifa Viti Vitatu Tanzania Bara Ndg. Shamira Mshangama akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa Jumuiya ya Vijana CCM na kuhamasisha ushiriki wa vijana kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025.

Shamira katika ziara yake ya Mkoani Simiyu amechangia pesa kwa kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Mkoa wa Simiyu  inayoongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Elias Nyasilu, kwa ajili ya kusapoti ujenzi wa nyumba ya katibu wa UVCCM mkoa wa Simiyu, pia alichangia ujenzi wa nyumba ya Katibu wa UVCCM Wilaya ya Bariadi kwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Bariadi Ndg. Tinana Masanja.

Amesisitiza kuwa pamoja na kazi zote tunazofanya lakini viongozi tunajukumu la kuzingatia ujenzi wa CCM na Jumuiya zake.
“Naamini nyumba hii ya Katibu wa UVCCM ikikamilika itaenda kupunguza baadhi ya gharama ambazo Jumuiya inaingia katika kumtafutia sehemu ya kuweka malazi
Mtendaji wetu wa vijana.

Mwisho, Shamira alipata wasaa wa kuzungumza na viongozi pamoja na wana CCM wa kata ya Nyangokolwa iliyopo katika Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kuwaasa juu ya kuendelea kuyasema mazuri anayoyafanya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani ya CCM kwenye maeneo yote wanayotoka ili kuhakikisha ushindi wa kutosha kwa Chama Cha Mapinduzi katika Uchaguzi mkuu 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *