MCHENGERWA AFANYA MAZUNGUMZO NA KAMPUNI YA JOSPONG UDHIBITI TAKA MIJINI

0

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa amefanya mazungumzo na wawakilishi wa JOSPONG group of companies ya nchini Ghana, kwa lengo la kujadili namna bora ya udhibiti wa taka na usimamizi wa usafi wa mazingira.

Waziri Mchengerwa amefanya kikao na JOSPONG group of companies katika ukumbi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI jijini Dodoma tarehe 14.02.2025 na kampuni hiyo imeonesha nia ya kuwekeza kwenye masuala ya huduma ya uthibiti wa taka na usimamizi wa usafi wa mazingira mijini.

Mhe. Mchengerwa amefanya kikao kazi na wawekezaji hao ili kuwa na uelewa wa pamoja juu ya shughuli wanazozifanya katika eneo la udhibiti wa taka na usafi wa mazingira, ili kuona kama kuna haja ya kushirikiana kwa kuzingatia maslahi mapana ya taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *