SHARIFA SULEIMAN MWENYEKITI MPYA BAWACHA TAIFA

0

Sharifa Suleiman ameibuka kidedea katika kinyang’anyiro cha nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) baada ya matokeo kutangazwa.

Sharifa ameshinda kwa kura 222 sawa na asilimia 62%  dhidi ya mpinzani wake Celestine Simba ambaye amepata kura 139 sawa na asilimia 38% idadi ya wapiga kura ni 382 huku halali zikiwa 361 na zilizoharibika zikiwa 2.

Sharifa ameshinda baada ya uchaguzi kurudiwa kutokana na matokeo ya awali kutokuwa na mgombea aliyefikisha kura zaidi ya asilimia 50%

Sharifa alikuwa Makamu Mwenyekiti wa BAWACHA Zanzibar na baadae kuwa Kaimu Mwenyekiti wa Bawacha Taifa.

Mkutano Mkuu wa BAWACHA umeanza Alhamis Januari 16, 2025 na umemalizika leo Jumamosi Januari 18, 2025

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *