CHADEMA YAMVUA CHEO MWENYEKITI WAKE WA SHINYANGA
Kamati Tendaji ya CHADEMA Kanda ya Serengeti inayoundwa na Mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga katika kikao chake cha jana Jumatano January 08, 2025 kilichofanyika Manispaa ya Shinyanga, kimefikia maamuzi ya kumvua Uongozi Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi kutokana na kukiuka maadili na utovu wa nidhamu ikiwemo kuchafua Viongozi wa Chama chake Kitaifa kupitia mitandao ya Kijamii.
Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi January 9 January, 2025 na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami, imesema “Tunapenda kuujulisha Umma kuwa, kuanzia sasa Emmanuel Ntobi siyo Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga”
Itakumbukwa mwaka 2023 Ntobi aliwahi kusimamishwa Uenyekiti wake kwa mwaka mmoja kutokana na makosa ya kinidhamu na hivi karibuni ameweka wazi mitandaoni kuwa anamuunga mkono na kumpigia kampeni Freeman Mbowe awe Mwenyekiti tena wa Chama hicho huku baadhi ya maandiko na kauli zake zikilalamikiwa na wanaomuunga mkono Mgombea wa Uenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu kuwa zinamkashifu Lissu.