WILAYA 139 KUFIKIWA NA HUDUMA YA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO

0

Jumla ya Wilaya 139 Nchini zita fikiwa na huduma ya   Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na mpaka sasa Wilaya 108 tayari zimefikiwa huku  Wilaya 31 zilizosalia nazo zikitarajiwa kupata huduma ya mkongo wa Taifa ifikapo mwezi Juni mwaka huu.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa  Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi wakati akihitimisha ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Pwani alipo tembelea na kukagua Vituo Vya Mkongo vilivyopo Chalinze, pamoja na kituo kipya  Cha Mkongo wa Taifa   kilicho jengwa Kibaha.

Aidha, Mhe. Mahundi  amempongeza na kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan  kwa namna anavvyo endelea kuiwezesha Sekta hii ya Mawasiliano apa Nchini Kwa kuendelea kuwekeza fedha nyingi katika Shirika la mawasiliano apa Nchini ( TTCL) na kuahakikisha  Shirika linakuwa kibiashara pamoja na kuifanya Tanzania kuwa ya kidijitali isibaki kama Kisiwa.

Vilevile, Mhe Mahundi ameeleza kuwa Serikali tayali imetenga fedha Kwa ajili ya ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kuelekea Nchi jiran ya Congo (DRC) kupitia Ziwa Tanganyinga hadi Kalemei na tayali Utekelezaji wake umeshaanza na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka mradi huu utakuwa umekamilika.

Sambamba na hayo, Mhe.Mauhidi amaeleza kuwa kazi kubwa inaendelea kufanyika katika uwekezaji wa Mkongo wa Taifa ikiwa ni pamoja na Kuunganisha Mkongo wa Taifa na Mikongo ya Baharini, kupitia SEACOM, EASSY na 2AFRICA, na kwakuzingatia tunajenga Tanzania ya dijitali tunaunganisha Mkongo wa Taifa na Mikongo ya Baharini iliyopo Mombasa Kenya kupitia HorohoroTanga. Na hii itasaidia kuongeza uhakika wa huduma ya Mawasiliano Nchini.

Endapo mkongo wa Taifa wa Mawasiliano utakamilika utapanua wigo kibiahara ndani na nje ya nchi na kuongeza uchumi wa kidijitali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *