WAZIRI MWIGULU AKIPOKEA ZAWADI MAKAMU MWENYEKITI WA CHENBA YA WAFANYABIASHARA NCHI ZA SAUDI ARABIA

0

Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lamdeck Nchemba Madelu (Mb), akipokea zawadi kutoka kwa Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara, Riyadh, nchini Saudi Arabia, Bw. Ajian Saad Al-jlan, kwa kutambua mchango wake katika kukuza biashara na masuala ya uwekezaji nchini Tanzania, kupitia wadhifa wake wa Waziri wa Fedha.

Tukio hilo limefanyika wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Biashara na Uwekezaji na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, Jukwaa lililoandaliwa na Serikali kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini humo, likiwa na lengo la kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo Tanzania kwa jumuiya ya wafanyabiashara wa Saudi Arabia ili kuvutia mitaji na teknolojia vitakavyochochea ukuaji wa uchumi na kukuza kipato kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Mawaziri wengine waliotunukiwa zawadi hizo ni Prof. Kitila Mkumbo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Suleiman Jafo, Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, Waziri wa Nchi Ofisi yar ais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji-Zanzibar, Mhe. Shariff Ali Shariff na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *