MBUNGE WA JIMBO LA IGUNGA MHE. NGASSA AONGOZA SAFU USHAMBULIZI TIMU MPIRA WA WAVU YA BUNGE
Mchezaji wa Timu ya Mpira wa Wavu (Volleyball) ya Bunge la Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa Ameongoza safu ya ushambuliaji ya Timu ya Mpira wa Wavu (Volleyball) ya Bunge la Tanzania dhidi ya Timu ya Bunge la Kenya. Timu ya Bunge la Tanzania imepata ushindi wa Seti Tatu kwa Moja (3 – 1) dhidi ya Kenya kwenye mchuano mkali uliochezwa kwenye Vijana vya Aghakhan Academy Mombasa Sports Arena.