MBUNGE MAVUNDE AWAOMBA WANADODOMA KUJITOKEZA KWA WINGI KUSHIRIKI UCHAGUZI

0

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amewaomba wana Dodoma kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi wa kuchagua viongozi wa serikali za mitaa ifikapo tarehe 27.11.2024. Mavunde ameyasema hayo jana katika mitaa ya Mnyampala-Bahi Road na Chololo-Kikombo wakati wa kampeni za kuwanadi wagombea uenyekiti na ujumbe wa serikali za mitaa.

Mh. Mavunde amepongeza juhudi kubwa inayofanywa na serikali ya awamu ya Sita chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt. Samia S. Hassan ya utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya maendeleo na hivyo kusaidia kutatua kero za msingi za wananchi. “Kero kubwa hapa Mnyampala ni suala la mifumo ya maji taka,tunao mradi wa kuboresha mfumo wa Maji taka utakaogusa kata 16 ikiwemo eneo hili,hivyo ni dhahiri kwamba kero yenu inakwenda kutatuliwa.

Hapa Chololo tumechimba kisima cha maji,tumebaki usambazaji wa huduma hii ili kuwafikia wananchi kwa uwingi,Mkandarasi ameshapatikana kutekeleza mradi huu“Alisema Mavunde Akihitimisha mikutano yake,Mbunge Anthony Mavunde amewataka wananchi kujitokeza kwa uwingi kushiriki uchaguzi huo tarehe 27.11. 2024 na kutumia fursa hiyo kuwaomba wawachague viongozi wa CCM wanaogombea uenyekiti na ujumbe wa serikali za mitaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *