TAKUKURU MKOA WA DODOMA YAWEZESHA HALMASHAURI YA JIJI KUKUSANYA MAPATO YA MIL308.6 NDANI YA SIKU KUMI
Katika kuimarisha ukusanyaji mapato ya Halmashauri za mkoa wa Dodoma Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU imefanya ufuatiliaji wa ukusanyaji ushuru wa huduma za leseni za biashara na mabango kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkurugenzi wa Jiji ambapo jumla ya Milioni 308.6 zilikusanywa ndani ya siku Kumi katika kata Tatu.
Akizungumza na Waandishi wa habari ofisini kwao Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Dodoma Victor Swella, kuhusu utendaji kazi wao katika kipindi cha Mwezi Julai – Septemba mwaka huu ambapo ametaja kata hizo kuwa ni Madukani, Uhuru na Majengo na makusanyo hayo yanatokana na leseni za biashara Milioni 107.5, Ushuru wa huduma Milioni 194.8 na ushuru wa mabango Milioni 6.