KAMBI YA MADAKTARI WA RAIS SAMIA KUMALIZA RUFAA ZA NJE ZA MKOA KAGERA

0

Kambi ya Madaktari Bingwa wa Rais Samia Suluhu Hassan Mkoani Kagera imeleta tija kwa kumaliza Rufaa zisiso za msingi za nje ya mkoa kwa asilimia kubwa kutokana na huduma za kibingwa zilizowezesha wananchi kupata huduma bora kwa gharama nafuu na kwa wakati katika maeneo yao.

Hayo yamebainishwa leo Novemba 4, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mhe. Etasto Sima kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Mhe. Fatma Mwassa, wakati wa kuwapokea madakatari hao.

Amesema madakatari bigwa watatoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi kwa wananchi wa mkoa wa Kagera kupitia hospitali za wilaya nane za mkoa huo.

Amesema Mkoa wa Kagera umepokea madaktari bingwa wa Rais Samia Suluhu Hassan ambao wameanza kambi rasmi ya kutoa huduma za matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi kupitia hospitali za wilaya za mkoa.

“Huduma hizi zitasaidia mkoa kumaliza rufaa za nje ya mkoa sisizo za msingi, wananchi kupata huduma bora za kibingwa na ubingwa bobezi na kuwapunguzia gharama za kwenda kupata huduma za kibingwa nje ya mkoa wa Kagera.

“Hii itasaidia sana kwasababu wengi wamezoea kwenda Bugando na sehemu nyingine lakini huduma hii ikitolewa hapa wananchi wengi watajitokeza kwani bado uhitaji ni mkubwa licha ya madaktari hao kufika kwa mara ya pili mkoani hapa,” ameeleza Mhe. Sima.

Amesema madakatari waliowapokea ni pamoja na madakatari bingwa wa watoto bobezi, watoto wachanga, magonjwa ya wanawake, magonjwa ya mfumo wa mkojo.

Wengine amewataja kuwa ni madaktari bingwa wa usingizi na ganzi salama, magonjwa ya ndani, magonjwa ya kinywa na meno, magonjwa ya upasuaji wa mifupa pamoja na wauguzi wakunga wabobezi.

Aidha amesemna huduma za upasuaji na matibabu ya kitaalamu kwa wagonjwa wenye matatizo ya mfumo wa mkojo, magonjwa ya ndani, huduma za wagonjwa kisukari,shinikizo la damu magonjwa ya moyo na mengineyo zitatolewa.

“Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutuletea madakatari bingwa na ubingwa bobezi nitoe wito kwa wananchi wenye uhitaji kufika kwenye hospitali zetu ndani ya mkoa wa Kagera kupata huduma hizi na kufanya uchunguzi wa afya zao,”amesema Mhe. Sima.

Kwa upande wake mwananchi wa mkoa huo Bi. Faustie Simon, amesema wanaishukuru Serikali kwa kuwezesha kampeni hiyo ambayo wananchi wa vijijini watanufaika kutokana na kupunguza gharama za kusafiri kufuata huduma.

Akizungumzia hali ya huduma za afya katika mkoa huo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Dkt. Samweli Laizer, amesema huduma za upasuaji zimeendelea kumarika kwa akina mama wajawazito na kupunguza vifo vya watoto wachanga na mama wajawazito.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *