AZANIA NI BENKI YA KIZALENDO – CPA. FELIX
“Benki ya Azania ni benki ya kizalendo hasa ukiangalia muundo wake na umiliki wake ambapo 99% inamilikiwa na mifuko ya jamii yani PSSSF, NSSF, NHIF, WCF na 1% inamilikiwa na EADB pamoja na wana hisa binafsi waanzilishi wa benki hii.
Kwa upande wa utendaji bodi na menejimenti wote ni wazawa, ni benki binafsı na ya kwanza kuanzishwa nchini mwaka 1995, benki hii imekuwa ikitoa huduma za kibenki kwa zaidi ya miaka 29 sasa, ikipanuwa wigo wake wa kibiashara mwaka hadi mwaka ambako hadi sasa ina matawi 25 nchi nzima.” CPA Felix Maagi Makamu mwenyekiti wa bodi amewasilisha waraka wake kwa mgeni rasmi Dkt. Mwigulu Nchemba katika hoteli ya Best western jijini Dodoma.