MAANA YA RAIS SAMIA KUIFUNGUA NCHI
Tangu aingie madarakani Machi 2021 hadi Agosti 2024, Rais Samia Suluhu Hassan ameufungua uchumi wa Tanzania kwa dunia na kujenga mazingira bora ya biashara za kimataifa.
Matokeo ya juhudi hizi yanaonekana wazi katika ukuaji wa biashara yetu kimataifa, kutoka USD 17.4 bilioni (Mauzo nje – $8.4bn, Uingizaji bidhaa – $9bn) hadi kufikia USD 31.4 bilioni (Mauzo nje – $15bn, Uingizaji bidhaa – $16.4bn). Hii ni sawa na ongezeko kubwa la 84%! 📈
Huku tukishuhudia ongezeko hili la kibiashara, deni la nje limeongezeka kwa asilimia 33%, kutoka $24.4 bilioni hadi $32.6 bilioni, ambalo ni jambo la kawaida kwa nchi zinazopiga hatua za kimaendeleo kupitia uwekezaji wa kimkakati.
Kwa kufanya hivyo, Rais Samia amefungua milango ya fursa mpya kwa Watanzania na kukuza uchumi kwa kuhakikisha Tanzania inakuwa sehemu ya ushindani wa kibiashara duniani.
Twende pamoja na Mama kwa maendeleo zaidi!
Chanzo benki kuu ya Tanzania monthly Economic Review May2021 and Monthly Economic Review for October 2024