MKUCHIKA AKAGUA NA KUZINDUA MAENDELEO MVOMERO
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum), Mhe. Kapt. George Mkuchika, Oktoba 27, 2024 ameweka jiwe la msingi katika ujenzi wa bweni, chumba cha darasa na vyoo matundu 13 katika Shule ya Sekondari Doma wilayani Mvomero katika mkoa wa Morogoro ambavyo vimegharimu zaidi ya shilingi milioni 143.
Waziri Mkuchika pia ameweka jiwe la msingi katika Zahanati ya Kijiji cha Mlandizi iliyopo wilayani humo ambayo imegharimu zaidi ya shilingi milioni 900, zahanati hiyo tayari imeanza kutoa huduma kwa wananchi.
Aidha, amezindua ujenzi wa mradi wa maji uliopo katika kijiji cha Mangae uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 643, ambao unahusisha ujenzi wa tanki la kuhifadhi maji, uchimbaji wa mtaro na ulazaji wa mabomba pamoja na ujenzi wa vituo 19 vya kuchotea maji.
Pia amefungua daraja katika barabara ya Doma shuleni – Kihondo lenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 44 na kukagua ujenzi wa boksi la karavati katika barabara ya Domakilosa – Maharaka.