ESTHER MATIKO; JASIRI WA KITAIFA NA KIMATAIFA/ MTETEZI WA MATATIZO YA TARIME MJINI
Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Esther Nicholas Matiko, amedhihirisha na kuthibitisha kuwa ni jasiri na shujaa katika siasa, uongozi na kitaaluma.
Mbunge huyu mpole kwa muonekano, lakini ‘mkali kichwani’, kila asimamapo kutoa hoja yoyote, ndani na nje ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hakika utapenda hoja zake, morali na umakini wake.
Siku zote licha ya kuwa Mbunge wa Viti Maalum, lakini Mheshimiwa Esther Nicholas Matiko, amekuwa kinara kutetea shida, mahitaji na matatizo ya wananchi wa Tarime Mjini.
Asimamapo Bungeni, kuzungumzia shida za Tarime Mjini, utadhani ndiye Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini, lakini hata hivyo amewahi kuluongoza Jimbo hilo, tangu 2015- 2020… Anakinua vyema.
Mhe. Esther Matiko, ndiye amegeuka mbeba shida na haja za Tarime Mjini!
Mbali na kuwasemea wananchi wa Tarime Mjini, Mhe. Esther Nicholas Matiko amekuwa kinara pia kwenye kutetea maslahi ya wananchi wa Taifa kwa ujumla!!!
Amekuwa akitetea maslahi ya watumishi wa uuma hususan askari polisi, Zima Moto na Magereza, stahiki na makazi yao kuboreshwa, huyu ni bingwa na mtetezi wa umma.
Mhe. Esther Nicholas Matiko, akiwa nje ya nchi, mathalan amefuatana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani ( IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Mhe. Matiko amekuwa akiwakilisha vyema mno Bunge na Taifa letu kwa hoja nzito za kidunia.
Nitaandika zaidi…. Mheshimiwa Esther Nicholas Matiko, anakumbukwa kwa machozi na wananchi wa Tarime Mjini.
Huwenda mwakani, Mungu akajibu maumivu ya wananchi wa Tarime Mjini, labda atagombea Ubunge, tuombe Mungu.
Nitaandika.
Endelea kufuatilia Uhondo TV, kwa habari na matukio mengi zaidi.
Imeandikwa na Brighton Masalu.