MAMA LISHE DODOMA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KWA KUREJESHA MIKOPO YA WAKINAMAMA

0

Wakina mama Lishe wa Stendi Kuu Jiji la Dodoma wamemshukuru Rais Samia S. Hassan kwa kurejesha tena mikopo ya 10% kwa ajili ya wakina mama,vijana na wenye ulemavu kwa kuwa wamekuwa wa wahanga wa mikopo ya riba ya juu(kausha damu) na hivyo kurejea kwa mikopo hii kwao ni ahueni kubwa sana.

Hayo yamesemwa leo katika hafla fupi ya kukabidhi meza za vyakula na majiko ya gesi yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde.

Akisoma Risala Katibu wa Mama Lishe Bi. Halima Mnene alimshukuru Rais Samia kwa kurejesha mikopo kwa wakina mama na kuahidi kutumia vyema mikopo hiyo ili kuimarisha na kukuza biashara zao.

Aidha,Mama Lishe hao wamemshukuru Mbunge Mavunde kwa namna ambavyo amekuwa nao karibu na kutatua changamoto zao ikiwemo utoaji wa meza na majiko kama nyenzo za kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma ya chakula.

Akizungumza katika hafla hiyo,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde amesema lengo la kutoka vifaa hivyo ni kuona mama lishe wa Stendi kuu Dodoma wanafanya biashara zao katika mazingira rafiki na kuwa na vifaa vya kisasa katika utoaji wa huduma ya chakula kwa abiria na wateja wengine wanaofika stendi hapo.

Naye Mkurugenzi wa Jiji wa La Dodoma Dkt. Fredrick Sagamiko amesema Jiji la Dodoma limetenga kiasi cha 4.5 bilioni kwa ajili ya kukopesha vikundi vya wakina mama ,vijana na wenye ulemavu na kuwataka mama Lishe hao kuchangamkia fursa hii.

Wakati huo huo katika kuboresha mazingira ya biashara katika eneo la
Stendi Kuu Dodoma Dkt. Sagamiko ameahidi kufanya mkutano na wadau wote wa stendi siku ya Jumatatu tarehe 21.10.2024 ili kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili.

Hafla hiyo ilitanguliwa na elimu na uhamasishaji wa kujiandikisha kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *