DKT. BITEKO ASHIRIKI ZOEZI LA KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA

0

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt Doto Biteko amewataka wakazi wa wilaya ya Bukombe Mkoani Geita kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la wakazi kwa ajili ya kupata nafasi ya kuchagua viongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu.

Dkt Biteko ametoa kauli hiyo mapema hii leo Oktoba 11,2024 baada ya kumaliza kujiandikisha katika daftari la mkazi katika Kituo Cha Bulangwa wilayani Bukombe Mkoani Geita huku akiwataka Wananchi kutosubiri hadi siku ya mwisho nabadala yake wajitokeze kwa wingi kujiandikisha ili wapate haki yao ya msingi ya kupiga kura.

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Bukombe Lutengano Mwalwiba amesema wanatarajia kuandikisha wananchi wapiga kura 191,124 na jimbo hilo linavituo 348 vyakupigia kura

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *