GEITA YATIKISA KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

0

Wananchi katika Wilaya za Mbogwe na Bukombe mkoani Geita wameipongeza Serikali ya awamu ya sita kwa kutekeleza miradi ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi na kuchochea upatikanaji wa maendeleo kwa kasi.

Hayo yamebainishwa jana Oktoba 8, 2024 katika muendelezo wa ziara ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo wilayani Mbogwe na Bukombe inayofanywa na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde mkoani Geita kwa niaba ya Mh. Rais Dkt. Samia S. Hassan.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa wilaya ya Mbogwe Dkt.Zakayo Sungura , alisema kuwa , kuanzia mwaka wa 2019/2020 mpaka kufikia mwaka wa 2024/2025 zaidi ya bilioni 2.7 zimepelekwa kwa ajili utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa hospitali katika kata ya Mbogwe.

Dkt.Sungura ameishukuru serikali kwa kukamilisha ujenzi wa hospitali ya wilaya pamoja na kupokea vifaa tiba vitakavyo saidi wananchi wa Mbogwe na maeneo ya karibu ambapo awali wananchi wa Mbogwe walisafiri umbali mrefu kupata huduma hizo.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo Mkuu wa Wilaya ya Bukombe Mhandisi Paskasi Muragili alisema kuwa kwa kipindi cha miaka 3 Wilaya ya Bukombe imepokea fedha za miradi ya maendeleo takribani shilingi bilioni 45 zimewekezwa kwenye sekta ya Afya, Barabara , Nishati ya umeme na sekta ya elimu.

Naye , Mkuu wa Mkoa wa Geita Mh. Martin Shigella amemshukuru Mh. Rais Samia kwa utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo ambayo imefikia kiasi cha shilingi bilioni 800 kwa katika kipindi cha miaka mitatu akibainisha kwamba kwamba miradi hiyo imesaidia kuchochea katika ukuaji wa kasi wa Mkoa wa Geita.

Kwa upande wake , Waziri Mavunde akizungumza na Wananchi wa Wilaya za Bukombe na Mbogwe
alisema kuwa Mkoa wa Geita ni kati ya mikoa iliyopokea fedha nyingi za miradi ya maendeleo kwenye nyanja ya Afya,Elimu,Miundombinu,Nishati ya umeme na uwezeshwaji wananchi kiuchumi ambayo kwa kiasi imechochea kukamilika kwa miradi ya maendeleo kwa kasi kubwa

Akielezea kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo , Waziri Mavunde alisema kwamba , Mhe. Rais Samia amefanya kazi kubwa sana mkoani hapa, hususan katika ujenzi wa shule mpya , Hospitali za Wilaya,Vituo vya Afya na Zahanati barabara mpya za lami,miradi ya maji na usambazaji wa nishati ya umeme vijijini.

“Ni dhahiri kwamba wanaGeita mtakubaliana na mimi kiasi cha Tsh 800 bilioni kilicholetwa mkoani hapa tunauona utekelezaji wa kweli wa miradi ya maendeleo” alisema Mavunde

Waziri Mavunde pia aliupongeza mkoa wa Geita kwa kuwa kinara katika kuchangia kwenye sekta ya madini ambapo kwa mwaka wa 2024/2025 imepanga kukusanya kiasi cha shilingi bilioni 246.

Waziri Mavunde yupo mkoani Geita kwa ziara ya kikazi ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo mkoani Geita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *