BONI YAI ASHINDA UENYEKITI AKIWA MAHAHABUSU

0

Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob ameshinda uenyekiti wa Kanda ya Pwani wa CHADEMA akiwa Mahabusu kwa kupata kura 60 sawa na 77% akimshinda Mpinzani wake Gervas Lyenda aliyepata kura 17 (23%) ambapo kwa ushindi huo sasa ataenda Mahakamani Jumatatu October 07,2024 kusikiliza hatima yake akiwa ni Mjumbe wa Kamati Kuu.

Kwa upande wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani kwenye uchaguzi huo Mshindi ni Ally Mohamed Kadogoo aliyepata kura 51 akimshinda Baraka Nandonde aliyepata kura 26.

Boniface anapokea matokeo hayo akiwa Mahabusu kufuatia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kupanga October 7, 2024 kutoa uamuzi juu ya dhamana ya Meya wa zamani wa Ubungo, Boniface Jacob baada ya October 01,2024 kutupilia mbali maombi ya Serikali juu kiapo cha ziada katika kiapo cha awali.

Jacob alifikishwa Mahakamani, September 19, 2024 na kisha kuwekewa pingamizi la dhamana katika kesi inayomkabili ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *