RAIS SAMIA ASHIRIKI TUKIO LA UZINDUZI WA KITABU CHA SOKOINE

0

Mapema leo katika katika uzinduzi wa kitabu kinachohusu Maisha na Uongozi wa Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1977 mpaka 1980 na 1983 mpaka 1984. Nafarijika kuona nchi yetu sasa inafanya kazi kubwa ya kuweka kumbukumbu, kuratibu, kutafiti, kutunza na kuchapisha maisha, changamoto na mafanikio ya viongozi wetu.

Mmoja ya mtumishi wa umma mahiri kabisa kuwahi kuitumikia nchi yetu, historia ya Hayati Sokoine inatukumbusha kwamba ukiwa mtu muadilifu hauhitaji kufukuzia vyeo bali kufanya kazi ya utumishi wako kwa bidii na uadilifu, na vyeo vitakufuata vyenyewe. Huu ndio msingi wa utumishi wa umma.

Historia za viongozi wetu hawa na machapisho ya kazi hizi iwe chachu kwa vizazi vyetu vya sasa na vijavyo kwenye mafunzo ya uongozi na historia ya nchi yetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *