SILLO AWAPONGEZA RSA KWA KUTOA ELIMU YA USALAMA BARABARANI

0

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Daniel Sillo, ametoa Rai kwa Viongozi wa Usalama barabarani na Viongozi wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kuwaunga mkono Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA) katika juhudi za kujali Usalama Barabarani pamoja na kutoa elimu ya usalama barabarani ili kuliongezea nguvu Jeshi la Polisi

Naibu Waziri amesama hayo katika maadhimisho ya miaka kumi ya Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA) yaliyofanyika mkoani Iringa Septemba 28, 2024.

Sillo amewapongeza Mabalozi hao kwa kuendelea kutoa elimu ya usalama barabarani ambayo ni muhimu katika kupunguza ajali zinazotokana na makosa ya kibinadamu.

“Elimu ya Usalama Barabarani ni nyenzo muhimu kwa kuwa Watu wakielimika, watapunguza kufanya makosa bila kufahamu na tutaendelea kuokoa maisha ya watu wengi,” Alisema.

Aidha, Mhe. Sillo alisema kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ipo katika hatua za mwisho za kuboresha Sheria za usalama barabarani. Aliahidi Muswaada wa Sheria hiyo utawasilishwa bungeni hivi karibuni ili kuhakikisha sheria hizo zinafanyiwa maboresho

Katika hatua nyingine, Sillo aliwataka madereva, hasa waendesha pikipiki, kuzingatia kanuni za usalama barabarani. Alisisitiza Mambo muhimu kwa Madereva kama vile kutotumia vilevi wanapokuwa wanaendesha, Kutokuendesha vyombo vya moto katika njia za waenda kwa miguu, Madereva wa Pikipiki kuvaa kofia ngumu pamoja na Abiria zao

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *