MAJENGO 67 YA HALMASHAURI YAMEKAMILIKA – WAZIRI MCHENGERWA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawalam za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema mpaka sasa majengo ya Utalawa ya Halmashauri 67 ujenzi wake umekamilika na majengo mengine 60 yapo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji.
Mhe. Mchengerwa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga lililozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan lililojengwa katika Kata ya Kigonsela wilayani mbinga leo tarehe 25.09.2024.
Amesema Mhe. Rais ulipoingia tu madarakani ulitoa shilingi Bilioni 206.24 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya utawala ya Halmashauri, nyumba za Wakurugenzi pamoja na nyumba za Wakuu wa Idara ili kuboresha mazingira ya kutolea huduma kwa wananchi.
Napenda kukufahamisha kuwa mpaka sasa majengo ya utawala 67 yamekamilika na sasa wananchi wanapata huduma karibu kabisa na maeneo yao.
Akizunguzumzia Jengo hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Joseph Kashushura Rwiza amesema jengo hilo limegharimu kiasi cha shilingi Bilioni 3.2 kati ya shilingi Bilioni 3.5 zilizokua zimetengwa na kiasi kikichobakia ni kwa ajili ua kazi ndogo ndogo zilizobakia.
“Mhe. Rais Jengo hili la Halmashauri lina jumla ya Ofisi 72 kwa ajili ya Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi, Wakuu wa Idara pamoja na Wasaidizi wao wote, na zaidi kuna kumbi 2 za Mikutano kwa ajili ya Mikutano ya Vikao vya Menejimenti na vile Kamati pamoja na Baraza la Madiwani’
Ameongeza kuwa Jengo limesaidia sana upatikanaji wa huduma kwani hapo awali Mkurugenzi pamoja na Wakuu wa Idara walikua wanakaa mbalimbali hivyo mwanancho kupata usumbufu wa kutoka Ofisi moja kwenda nyingine lakini kwa sasa huduma zote zinapatikana ndani ya jengo moja’ alisisitiza Kashushura.