MILIONI 780 KUBORESHA HUDUMA YA MAJI MARANGU MASHARIKI

0

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Moshi ( MUWSA) imekusudia kutekeleza mradi wa majisafi wenye lengo la kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi kwenye vijiji vya Samanga, Rauya pamoja na Ashira vilivyoko kwenye Kata ya Marangu Mashariki Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro,

Mradi huo unategemewa kuzalisha mita za ujazo lita 4,320 kwa siku utahudumia zaidi ya wananchi 10,574.

Mradi huo utakaotekelezwa kwa awamu mbili zikihusisha kuboresha vyanzo viwili vya maji vya Kerya pamoja na Lyasongoro, ulazaji wa bomba kuu la usambazaji majisafi umbali wa kilomita l7.35 kutoka kwenye vyanzo hadi eneo la tanki la maji la Samanga Makao Makuu.

Mradi huo unategemea kukamilika Oktoba, 2024 kwa awamu ya kwanza na utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi huo itaanza Novemba 2024 na kukamilika Januari 2025 itakayohusisha uchimbaji pamoja na ulazaji wa bomba yenye vipenyo mbalimbali ili kuwasogezea wananchi huduma pamoja na ujenzi wa vituo vipya vya kupunguza kasi ya maji yaani BPT

Mamlaka imeshirikiana na wananchi na viongozi wa Kata hiyo kama wanavyobainisha kwenye ziara ya Kamati ya Maendeleo ya Kata ilipotembelea na kujionea utekelezaji wa kazi mbalimbali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *