RAIS SAMIA ARIDHISHWA NA UJENZI WA KIWANJA CHA NDEGE SONGEA

0

Kukamilika kwa uboreshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Songea kumefanya Mkoa wa Ruvuma kuwa kitovu muhimu cha biashara kwani idadi ya abiria imeongeza kutoka abiria 3,000 hadi kufikia 19,000 wanaoshuka Mkoani Ruvuma kwa kuwa hivi sasa ndege zinashuka mara tatu (3) kwa wiki.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo leo Septemba 23, 2024 katika Kilele cha Tamasha la Tatu la Utamaduni lililofanyika katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea Mkoani Ruvuma.

“Nimeridhishwa sana na ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Songea uliofanyika na kwamba Songea sasa inakwenda kuwa kitovu muhimu cha biashara kwasababu idadi ya wanaokuja Songea imeongezeka sana”, Amesema Dkt. Samia.

Dkt. Samia ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Ruvuma kuchangamkia fursa zinazotokana na uwepo wa Kiwanja hicho cha Ndege cha Songea.

Dkt. Samia ameeleza kuwa tangu mwaka 2021 Serikali imekuwa ikitoa fedha nyingi katika Mkoa wa Ruvuma kwa ajili ya utekelezaji wa maendeleo ya kijamii ikiwemo Shule, Hospitali, Maji pamoja na utekelezaji wa miradi mikubwa itakayokuza uchumi ikiwemo barabara, bandari, Kilimo na Madini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *