MTANZANIA MWENYE UWEZO WAKUSHIKA NYUKI

0

Wahenga walisema tembea uone ndivyo unaweza kusema , hii ni baada ya maajabu ya kipeeke aliyonayo kijana Athuman Masimba mwenye umri wa miaka 30 mkazi wa Geita ya kukamata kundi la nyuki kwa mikono yake bila kudhurika huku akifurahia kile anachokifanya hasa cha kusaidia wananchi pale nyuki hizo zinapohamia kwenye makazi yao.

Masimba anasema ujarisi huo wa kamata nyuki aliupata kwa kujifunza namna ya kufunga nyuki kisasa na pale inapoekea nyuki wamefika katika makazi wa watu huwaondoa na kuwarejesha msituni ambako ndiko makazi huo huku akijipatia kipato kutokana na kufanya kazi hiyo.

Pia amesema watu wengi huzani anatumia dawa kuwakamata nyuki hao lakini kwakwe anasema ni ujuzi tu ndio anautumia pamoja na mafunzo aliyopatiwa kuwakamata nyuki hao bila kuleta madhara huku akisema mwanzoni kipindi anaanza kazi hiyo aling’atwa lakini kwasasa haipo hivyo japo ikitoa husema ni ajari kazini.

Kwa upande wao mashuhuda wa takio hilo wamesema ni maajabu kuona mtu anakamata nyuki bila kung’atwa huku wakimsifia kwa kujipatia ajira ambayo inamuingizia kipato.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *