WANANCHI PERAMIHO WALIPUKA KWA SHANGWE KUPATA MAJI,WATUMA SALAMU KWA RAIS SAMIA

0

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso amepokelawa kwa Shangwe Jimbo la Peramiho ambapo amezindua Mradi wa Maji Kijiji cha Kizuka Halmashauri ya Wilaya ya Songea wenye gharama ya Shilingi Milioni 730.4 unaolenga kuwahudumia wananchi wapatao 6,005 wa kijiji hicho.

Akiongea na Wananchi wa Kizuka Jimbo la Peramiho Mhe. Aweso amewahakikishia kuwa Serikali ya Dkt. Samia imejipanga kumaliza kabisa changamoto ya upatikanaji wa majisafi na salama huku akisisitiza suala la utunzaji wa miundombinu ya mradi huo.


Wananchi wametuma salamu za shukrani kwa Mhe Skt Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza ahadi yake ya kuwatua kina Mama wa Peramiho ndoo kichwani.

Awali akitoa salamu za Pongezi kwa Njia ya Simu Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Jenista Mhagama (Mb) ambaye pia ni Waziri wa Afya ameishukuru sana Serikali ya Awamu wa sita kwa kutekeleza miradi mingi ya maendeleo katika Jimbo lake .

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *