WANANCHI TANDAHIMBA WAFUNGUKA KUWASOGEZEA HUDUMA ZA KIBINGWA
Wananchi wa mkoani Mtwara wilaya ya Tandahimba wamshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwasogezea Huduma za kibingwa na Bingwa Bobezi karibu na kuwawezesha kutosafiri umbali mrefu kufuata Huduma.
Shukrani hizo zimetolewa leo na baadhi ya Wananchi walio jitokeza kupata Huduma kwa madaktari bingwa wa Rais Samia walioweka kambi ya siku Sita katika halmashauri tisa za mkoa wa Mtwara.
Miongoni mwa wakazi waliofika katika Hospitali ya Mji Nanyamba , ni Mohammed Issa (29) ambaye amempongeza Rais Samia kwa hatua ya kuwafikia wananchi wa ngazi ya msingi ukizingatia wao kipato chao ni cha chini na Huduma hizi za kibingwa na bingwa bobezi ili waweze kuzipata ilikuwa wasafiri umbali wa mwendo mrefu na kutumia gharama kubwa kufata Huduma hizo.
“Hakika kambi hii ya ujio wa Madaktari Bingwa wa Mama Samia kutufikia katika maeneo yetu ni ishara tosha ya utendaji mzuri na uwajibikaji wa kiongozi wetu kwa wananchi wake ili kuhakikisha tunakuwa na afya bora kwajaili ya kuendelea kulitumikia taifa kwa shughuli za utafutaji wa maendeleo”, ameeleza Ndugu Issa.
Kwa upande wake Bwana Hamisi Malela Mnandaje (47) mkazi wa Wilaya ya Tandahimba ametoa wito kwa wananchi wenzake kuhakikisha wanakata bima ya afya mara baada ya mauzo ya zao la korosho ili kuwa na uwakika wa matibabu kwani serikali chini ya uongozi wa Rais Samia umefanya uwekezaji mkubwa katika sekya ya afya ikiwemo kuhakikisha madaktari bingwa na bingwa Bobezi wanafika katika ngazi ya msingi na wananchi waweze kupata Huduma hizo katika maeneo yeo.
“Tunamshukuru Rais Samia kwa kutoa jopo la madaktari bingwa kuja wilayani kwetu kutuhudumia sisi wananchi wake ili tuwe na afya njema katika utafutaji wetu wa kila siku”, ameshukru Bwana Mnandaje
Aidha Bwana Mnandaje ametoa wito kwa wanamtwara wote kujitokeza kwa wingi katika vituo vya kutolea Huduma za afya vilivyotangazwa ili kupata Huduma za kibingwa na bingwa bobezi kutoka kwa madaktari wa bingwa wa Rais Samia kwani zimesogezwa katika maeneo yeo hivyo ni jukumu la kila mwenye uhitaji wa matibabu kuchangamkia fursa kwani inasaidia kupunguza gharama zisizo za msingina kusafiri mwendo mrefu kufata Huduma hizo katika hospitali za Taifa, Kanda na Mikoa .