MTUMBIWI WAZAMA WATU 6 HAWAJULIKANI WALIPO

0

Watu sita hawajulikani walipo baada ya mtumbwi waliokuwa wakisafiria kutoka katika Kijiji cha Mwiruruma kuelekea Kitongoji cha Bulomba wilayani Bunda mkoani Mara kuzama katika Ziwa Victoria.

Habari kutoka wilayani Bunda zinaeleza kuwa tukio hilo lilitokea jana Septemba 15, 2024 majira ya jioni
huku chanzo kikitajwa kuwa ni kuzidisha uzito.

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt. Vicent Naano amethibitisha kutokea kwa tukio na kueleza kuwa mtumbwi huo unadaiwa kubeba watu 16 na baada ya kuzama watu tisa waliokolewa wakiwa hai, mwili mmoja uliopolewa na watu sita hawajulikani walipo hadi sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *