SUMAJKT KULAMBA MIRADI MINGINE YA REA

0

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko amelipongeza Shirika la Uzalishaji Mali la JKT(SUMA JKT) kupitia SUMAJKT Electric Co.Ltd kwa kukamilisha miradi ya kusambaza umeme vijijini haraka na kwa wakati husika.

“Katika Wakandarasi wanaotupa fahari sisi Wizara ya Nishati ni SUMA JKT chini ya Brigedia Jenerali Petro Ngata, miradi yao wamemaliza kwa haraka na kwa muda hivyo SUMA JKT wanastahili kupewa miradi mingine mingi kwa sababu usimamizi wa miradi yao wanayoifanya inatupa heshima sisi kama Serikali” alisema..Dkt.Biteko

ameyasema hayo Septemba 13,2024 jijini Dodoma wakati akizindua jengo la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kushuhudia utiaji saini wa mkataba wa kuwezesha miradi ya nishati safi ya kupikia katika makambi 22 ya JKT kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)

Aidha, Dkt.Biteko amesema kuwa wanakwenda kwenye miradi ya kupeleka umeme katika vitongoji mbalimbali hapa nchini, hivyo amemtaka Mwenyekiti wa Bodi ya REA pamoja na menejimenti, kuhakikisha kwamba kama kuna mahali panahitaji kazi ya dharura na ya haraka wapatiwe SUMA JKT.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *