Klabu ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa mkondo wa kwanza kuwania kuingia hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Katika mchezo huo uliochezwa Ethiopia, Yanga wakiwa ugenini wamepata ushindi wa Goli moja pekee lililofungwa na Prince Dube Dk 45 kipindi cha Kwanza.

Hivyo Yanga atahitaji kupata Suluhu au sare ya aina yoyote katika mchezo wa marejeano Visiwani Zanzibar Septemba 21, 2024 ili kusonga mbele Kwa kuingia hatua ya Makundi.

Licha ya ushindi wa Leo, bado Yanga hawakuwa makini katika kutumia nafasi ambapo wamekosa mabao mengi ya wazi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *