MSIWAFICHE WATOTO WENU WENYE ULEMAVU

0

Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Dododoma Mhe.Fatma Toufiq amewataka wazazi na walezi wenye watoto wenye ulemavu kutowaficha watoto wao ndani akisema kufanya hivyo ni kuwanyima haki zao za msingi.

Mhe. Toufiq ametoa kauli hiyo kwenye mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi Buigiri wasioona iliyopo katika wilaya ya chamwino mkoani Dodoma. ambapo amehahidi kuwalipia bima ya afya wanafunzi 80 katika shule hiyo

Amesema kuwa watu wenye ulemavu wana haki sawa na watu wengine hivyo inapaswa kushirikishwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi pamoja na fursa ili waweze kujikwamua kiuchumi na kutoa mchango wao katika maendeleo ya Taifa.

“Inabidi kutoa Elimu kwa Jamii na Familia watambue kuwa watoto wenye Ulemavu wapewe fursa ya Elimu kwani wakipewa Nafasi wanafanya Vizuri sana katika kutekeleza Majukumu yao, mlemavu haina maana kwamba ukate tamaa ya Maisha hapana endeleeni kupambana mimi naamini kwa uwezo wa mwenyezi mungu ndoto zenu zitatimia “

Aidha Amempongeza Rais Dkt.Samia kwa kuendelea Kuwapa Fursa walemavu katika Nafasi Mbali Mbali pia kwa kuhakikisha Ustawi wa watu wenye Ulemavu unapewa kipau Mbele katika taifa letu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *