WAZIRI AWESO AMEMWAGIZA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAJI ENG. MWAJUMA
Waziri wa maji Jumaa Aweso amemwagiza katibu mkuu wa wizara ya maji Eng Mwajuma Waziri kuwapatia kiashi cha shilingi million 10 Mkurugenzi wa GEUWASA na Meneja wa RUWASA mkoani geita kwa kazi nzuri waliyofanya ya kakamilisha miradi ya maji kwa wakati na kusaidia wananchi wa maeneo hayo kuondokana na adha ya maji.
Ametoa maagizo hayo katika uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa maji Bwanga wilayani Chato mkoani Geita ambao umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.6 na utawanufaisha wananchi elf 27 pamoja na taasisi mbalimbali, ambapo amesema viongozi hao wamefanya kazi kubwa katika maeneo yao hivyo wanasitahili pongezi huku akisisitia kuendelea kuziona juhudi zao katika miradi mingine.
Pamoja na hilo waziri wa maji Mh Jumaa Awezo amemwagiza katibu mkuu wa wizara hiyo pamoja na wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijiniRruwasa makao makuu kuja na mfumo mpya wa malipo ya Ankara za maji katika jumuiya za watumiaji maji nchini ili kuondokana na mfumo mpya wa malipo wa GPG ambao umeonekana kuwa kero kwa wananchi kutokana na kusababisha wananchi kukosa maji katika maeneo yao.
Meneja wa Ruwasa wilaya ya Chato amesema mradi huyo wa bwanga umegharimu zaidi ya shilingi bilioni moja na nusu na utawafikia zaidi ya wananchi elfu ishirini na saba huku akisema mradi huo utarajiwa kukamilika mwezi wa kumi na kuanza kutoa huduma kwa asilimia 100 katika vijiji viwili ambavyo vitanufaika na mradi huo.
Mbunge wa jimbo la chato Dokta Medard Kalemani amesema wamepokea zaidi ya billion 43.78 za kutekeleza miradi ya maji katika kipindi cha mika mitatu na kusema kukamilika kwa mradi huo kutawawezesha wananchi kutotumia maji yasiyo safi na salama kutoka kwenye mabwawa na visima vya asili.