PROF. JAY MZIMA WA AFYA, PUUZENI
Msanii Legendary wa Bongofleva Joseph Haule hajafariki kama ilivyoandikwa na baadhi ya Watu mitandaoni, ni mzima wa afya na ameiambia AMPLIFAYA ya CloudsFM kwamba yuko sawa kiafya na anazidi kuimarika.
Akiongea kwa simu na Mtayarishaji wa Vipindi CloudsFM @askofutza Profesa amenukuliwa akisema yafuatayo ”Ni habari ambayo haina ukweli wowote mimi ni mzima wa afya, mimi siumwi hata mafua…. Watanzania wapuuzie huu uzushi uliotokea, lakini nilishaimba nimeshazushiwa sana nimekufa eti nimepata ajali, washindwe na walegee Mwenyenzi niepushie mbali”Profesa Jay.