MZEE MAGOMA ASHINDWA KESI
Jumatatu Septemba 09. 2024 Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam imetupilia mbali maombi ya rufaa yaliyowasilishwa na Mzee Juma Magoma na wenzake dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Yanga SC, ambapo waleta maombi walikuwa wanapinga maamuzi ya shauri la msingi lililoamuliwa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Katika viunga vya Mahakama hiyo Mawakili wa pande zote mbili (2) wamezungumzia walivyopokea maamuzi hayo.