WAZIRI AWESO HUDUMA YAKUUNGANISHA MAJI IWE KWA SIKU 7

0

Waziri Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amewasisitiza watendaji wa sekta ya maji kuacha kukaa ofisini na badala yake kwenda kutatua kero za wananchi ikiwemo kushughulikia swala la upotevu wa Maji.

Mhe Aweso ameyasema hayo katika kikao kazi na Mamlaka za serikali za mitaa kujadili hali ya upatikanaji wa Maji katika jiji la Dodoma leo Septemba 5,2024

Aidha amesema kuwa huduma ya kuwaunganishia maji wananchi iwe ndani ya siku saba pale mwananchi anapokuwa amekamilisha maombi ya kuunganishiwa maji .

“Mwananchi aunganishiwe maji ndani ya siku saba Mara baada ya kukamilisha maombi ya maunganisho mapya “

Wakati akihitimisha hotuba yake waziri Aweso ameiagiza Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kuendeleza uchimbaji wa visima katika maeneo ya pembezoni ili kuongeza hali ya upatikanaji wa huduma ya maji katika jiji la Dodoma pamoja na ushirikishwaji wa wananchi katika ujenzi na usimamizi wa miradi ya maji .

Wadau walio hudhuria katika kikao hicho ni pamoja na watendaji wa Mitaa, wadau wa maendeleo Dodoma na Taasisi za Kisekta EWURA, Tanesco, RUWASA, TARURA, na TANROAD.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *