JOKATE ATEULIWA NA ASKOFU KURATIBU UKARABATI LIKONDE SEMINARI MBINGA

0
IMG-20250626-WA0126

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Jokate Mwegelo ameteuliwa na Askofu John Chrysostom Ndimbo wa Jimbo Katoliki la Mbinga kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu upatikanaji wa fedha na vifaa kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Likonde Seminari ambapo KM Jokate June 25,2025 amefika Mbinga na kumuhakikishia Askofu Ndimbo kwamba amekubali uteuzi huo na atahakikisha anaratibu ili kukusanya Tsh. bilioni 1.5 ambayo inahitajika ili kuzikabili changamoto zinazoikabili Seminari hiyo.

KM Jokate amesema “Tumekuja hapa baada ya kupokea barua ya kutuomba tushirikiane na Jimbo la Mbinga kupitia Baba Askofu Ndimbo kwamba kuna Likonde Seminari ambayo inatimiza miaka 65 mwaka huu na sisi ni Wadau wa Wilaya hii ya Mbinga basi tushirikiane kuona jinsi gani tutafanya ukarabati, binafsi naiona Seminari hii kama nembo ya Mbinga, tumekuja kuona mazingra baada ya kupokea barua ili kuboresha pawe rafiki kwa Vijana wanaokuja kupata elimu, nakupongeza Baba Askofu na tunakutia moyo mungu aendelee kukutumia kwa ajili ya Wana Mbinga

Seminari ya Likonde kwa zaidi ya miaka 60 imekuwa ikihudumia Jamii
kubwa ya Kitanzania hasa kwa wenye kipato cha chini lakini kwa sasa Shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya uchakavu mkubwa wa miundombinu yake ikiwemo madarasa, ofisi, mabweni, maabara, maktaba, mifumo ya maji na vyoo hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa mazingira ya ujifunzaji ambapo akiongea leo Askofu Ndimbo amemshukuru KM Jokate kwa kukubali kuongoza uhamasishaji huo ili kuwasaidia Wanafunzi wengi zaidi.

Wadau wengine wa Mbinga wakiwemo Viongozi ambao wameteuliwa kuratibu ukarabati huo ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda ambaye ni Katibu wa Kamati ya ukarabati  pamoja na Wajumbe wa Kamati akiwemo Mbunge wa Madaba, Dkt. Joseph Kizito, Mbunge wa Mbinga Vijijini, Beneya Kapinga, Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, Judge Dunstan Ndunguru , Faustine Njelekera na aliyekuwa DC Tarime, Glorious Luoga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *