NHC YAKABIDHI RASMI ENEO LA SANAWARI KWA BoT

Shirika la Nyumba la Taifa leo limefanya makabidhiano rasmi ya Kiwanja Na. 31-36, Kitalu Na. 3 kilichopo Sanawari, Arusha kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa ajili ya matumizi ya Serikali.
Makabidhiano haya yamefanyika na Mkurugenzi wa Sheria Bi. Sara Massamu kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NHC, yakihitimisha safari ndefu iliyojawa na mazungumzo ya kisheria, uratibu wa kiufundi na kazi ya pamoja kutoka timu mbalimbali ndani ya Shirika na Benki Kuu. Hatua hii ni ushuhuda wa dhamira ya kweli ya NHC katika kutekeleza majukumu yake kwa manufaa ya Taifa na kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Bi Sara alisema kuwa taaisisi hizo zinaamini kwamba ushirikiano huo kati ya NHC na BoT ni mfano mzuri wa mashirikiano ya taasisi za umma kwa maslahi mapana ya maendeleo ya Taifa.



