BALOZI DKT. NCHIMBI AHIMIZA KAMPENI YA TUTUNZANE ITUMIKE NCHI NZIMA


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amewahimiza wafugaji na wakulima kote nchini kuitumia kampeni ya Tutunzane ambayo imelenga kuimarisha maelewano na ustawi kati ya wakulima na wafugaji na kuondokana na migogoro ya matumizi ya ardhi.
Balozi Dkt. Nchimbi amesema hayo leo Juni 15, mwaka 2025 katika eneo la Nyakabindi Wilaya ya Bariadi Mkoa wa Simiyu wakati akifungua Kongamano la wafugaji kwa mwaka 2025 ambapo amehimiza kampeni hiyo itumike nchi nzima kuimarisha umoja wa jamii ya wafugaji na wakulima.
” Kampeni hii ya tutunzane iliyoanzishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero imeonyesha thamani ya wafugaji na wakulima kwa kuimarisha maelewano baina yao kwani sisi sote ni taifa moja, hivyo kampeni hii ya tutunzane itumike nchi nzima ili wafugaji wote wanufaike” alisema Balozi Dkt. Nchimbi.

Aidha Balozi Dkt. Nchimbi ameogeza kwa kusema kuwa Chama cha Mapinduzi kinadhamira ya kuinua ufugaji kwakutambua sekta ya mifungo ni sekta muhimu katika ukuwaji wa uchumi na kuzalisha ajira kwa vijana hivyo kitaenedelea kutoa kipaubele lengo ikiwa ni kuimarisha na kuwezesha upatikanaji wa ufugaji wa kisasa.
Katika hatua nyingine Balozi Dkt. Nchimbi ameipongeza serikali kwa kuiongezea fedha kweye bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kufikia bilioni 476.6 mwaka huu wa fedha 2025/2026 jambo litaisaidia wizara kutekeleza miradi ya sekta za mifugo na uvuvi.
