MCHECHU AIGALAGAZA KAMPUNI YA MWANANCHI, KULIPWA BILIONI 2.5

0
InShot_20250604_225910842

Mahakama ya rufani leo Tarehe 4 June 2025, imetupilia mbali maombi ya rufani namba 658 ya 2023 yaliofunguliwa na kampuni ya Mwananchi communication na the Editor Citizen News Paper, na kukubaliana na uamuzi wa Mahakama kuu kwenye kesi  Namba 48 ya 2021 kati ya Mwananchi communication na the Editor Citizen News Paper dhidi ya Nehemia Kyando Mchechu uliosomwa tarehe 3 March 2023 mbele ya Jaji Mgonya. 

Katika uamuzi huo wa mahakama ya rufani uliotolewa na Majaji watatu akiwemo Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Rehema Kerefu, Jaji Omar Othman Makungu na Jaji Dkt. Benhajj Masoud, mahakama ilipitia hoja tatu za msingi yaani, 1) kama mahakama kuu ilikuwa na uwezo wa kusikiliza shauli hili, 2) kama mdai aliweza kuthibitisha madai yake ya kudhalilishwa, 3) kama mahakama ilitumia utaratibu sahihi kutoa nafuu ambazo zilitolewa na mahakama kuu. 

Majaji wa mahakama ya rufani walikubaliana na hoja za wakili wa utetezi wa mjibu maombi  Advocate Aliko Harry Mwamanenge na kuona kwamba hakika mahakama kuu ilikuwa na uwezo wakusikiliza kesi hiyo na kwamba mjibu rufani alifanikiwa kudhibitisha madai yake ya kudhalilishwa na pia mahakama kuu ilitumia utaratibu sahihi kufikia tuzo ambayo ilitoa.

Kwakuzingatia mazingira hayo, mahakama ya rufani haikuona sababu ya kubatilisha au kubadilisha chochote kwenye maamuzi ya mahakama kuu na hivyo kuyabariki maamuzi hayo kama yalivyo.

Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd ilipewa hukumu ya kumlipa Bw. Nehemiah Mchechu, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Shilingi Bilioni 2.5 kwa kuandika habari za kumdhalilisha kwenye gazeti lao la The Citizen la Mchi 23 Mwaka 2018.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *