JARIDA LA TANAPA LANG’ARA MKUTANO MKUU CCM


Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limeonesha kwa vitendo namna lilivyotekeleza ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi(CCM), 2020-2025 kwa uweledi na ufanisi mkubwa.
Jarida hilo ambalo lilisambazwa kwa wajumbe wa mkutano mkuu, wageni na waalikwa limeonesha namna TANAPA ilivyotekeleza ilani hiyo na kupata mafanikio na upekee wa vivutio vya utalii nchini.
Katika nyakati tofauti wajumbe hao walionekana wakiperuzi jarida hilo katika makundi mbalimbali na wengine wakiwa mmoja mmoja.



