ANUSURIKA KIFO WAKATI AKIJARIBU KUHUJUMU MIUNDOMBINU YA TANESCO SINGIDA

0
IMG-20250528-WA0002

Kijana mmoja aliyejulikana kwa Jina la Rajabu Jumanne Mkazi wa Kijiji cha Njirii Kata ya Aghondi Wilaya ya Manyoni Mkoa Singida amepoteza nguvu ya kutembea baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakati akiwa anaiba nyaza za Umeme katika Transforma iliyopo katika kijiji hicho.

Akielezea tukio hilo leo tarehe 27/05/ 2025 Afisa Mtendaji wa kijiji hicho cha Njirii Adam George ambapo limetokea tukio hilo amesema kuwa alipata taarifa kutoka kwa wananchi wema muda wa saambili asubuhi na kumueleza kuwa kuna mtu amedondoka kwenye mnara wa YAS na alipofika alikuta mtu huyo ameshindwa kutembea na yupo kwenye Transforma ambalo lipo karibu na mnara wa YAS baada ya kumuhoji alikiri kuwa alikuja kuiba waya wa kopa na akishaiba huwa anasafirisha kupelekea Mwanza na sio mara yake ya kwanza kufanya hivyo na baada ya yeye kumuhoji aliwasilina na kituo cha polisi na wakafika katika eneo la tukio kwa ajili ya upelelezi.

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo Emanuel Soghweda amesema kuwa vitendo vya uhalifu havikubaliki katika jamii na kuwataka vijana ambao ni nguvu kazi katika jamii kufanya kazi halali za kuwaingizia kipato.

Mhandisi wa Shirika la umeme Mkoa wa Singida TANESCO Wilaya ya Manyoni Vicent Temba amesema kuwa watu wasiokuwa na nia njema wameiba miundombinu ya TANESCO ambapo wamefanya uharibifu mkubwa akisema zaidi ya Transforma tati zimefanyiwa uharibifu.

Kwa upande wa mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa ni jambo la kusikitisha kwa vijana kukosa uzalendo na kuanza kuhujumu mali za umma hivyo inapaswa vijana kujituma na kujafanya kazi za halali za kujiingiza kipato na kuleta maendeleo kwao binafsi na Nchi kwa Ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *