WAJUMBE WA BODI MFUKO WA TAIFA WA MAJI, WATEMBELEA NA KUKAGUA MRADI WA UJENZI WA JENGO LA OFISI ZA MFUKO NJEDENGWA


Wajumbe wa Bodi Mfuko wa Taifa wa Maji wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo Mhandisi Abdallah Mkufunzi wametembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujezi wa jengo la ofisi za Mfuko wa Taifa wa Maji katika eneo la uwekezaji Njedengwa jijini Dodoma mei 23.2025.
Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Maji Mhandisi Abdallah Mkufunzi ameridhishwa na maendeleo mradi huo.

Naye Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Maji Wakili Haji Nandule amesema ujenzi wa jengo hilo umeanza tangu Novemba 2024 huku ukitarajiwa kukamilika Mei 19.2026 na kugharimu Tsh.Bilioni 5.6 hadi kukamilika kwake.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka kampuni ya Group six international company limited Venance Masue amesema ujenzi wa mradi huo umefikia asilimia 15 huku wakitarajia kukamilisha ifikapo Mei 2026.

