WAZIRI CHANA: MPANGO MPYA KULETA MAGEUZI SEKTA YA NYUKI

0
IMG-20250520-WA0237

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt.Pindi Chana amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau imekuja na mpango wa kuendeleza sekta ya ufugaji nyuki ya Tanzania uliobora unaolenga kuongeza uzalishaji wa asali nchini.

Akizungumza kwenye kilele cha siku ya nyuki duniani jijini Dodoma, Dkt.Chana alisema mpango huo unalenga kuongeza kiwango cha uzalishaji wa asali kutoka tani 34,861 za sasa hadi kufikia tani 75,000 ifikapo Juni, 2035 na kuongeza mauzo ya mazao ya nyuki katika masoko ya kikanda na kimataifa.

Aidha, amesema kupitia Mpango huo takribani ajira mpya 43,055 zinatarajiwa kuzalishwa hasa kwa vijana na wanawake.

Awali, amesema pamoja na mafanikio mbalimbali bado sekta ya ufugaji nyuki inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo kiwango kidogo cha uzalishaji wa asali ikilinganishwa na uwezo uliopo.

“Kiwango kidogo cha asali kinachouzwa katika masoko ya nje ya nchi; kuendelea kwa matumizi ya mzinga ya asili ambayo huchangia katika uharibifu wa misitu; uvamizi wa maeneo ya hifadhi ambayo ndiyo makazi ya asili ya nyuki na matumizi ya viwatilifu vinavyoathiri afya ya nyuki,”amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *