MKUU WA IDARA YA MECHANJZATION AMETEMBELA MAMBANDA YA CHAI KWENYE MAONESHO YA SIKU YA CHAI DUNIANI

Mkuu wa Idara ya Mechanization -Wizara ya Kilimo, Injinia Anna Mwangamilo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara, ametembelea mabanda ya Waadau mbalimbali wa chai wanaoshiriki kwenye Maonesho ya Siku ya Chai Duniani yanayoendelea katika Uwanja wa Nyerere Square.

Akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania (TBT), Beatrice Banzi wametembelea maonesho hayo ambapo wamejionea matukio mbalimbali yanayoendelea.
Pia Injinia Anna alipata wasaha wa kukabidhi zawadi ya mitungi ya gesi kwa washindi 10 wa shindano la kupika chai lililoandaliwa na kampuni ya Maanjumat Group.

Pia katika Maonesho hayo zipo kampuni kadhaa za chai na za watoa huduma ya chai kama Chef Asili, Afritea, Kazi Yetu, Mponde na Shirika la Care

