KAMATI YA BUNGE YA BAJETI YAPOKEA TAARIFA YA MFUKO WA TAIFA WA MAJI


Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Taifa wa Maji Wakili Haji Nandule amewasilisha taarifa ya utolewaji wa fedha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge la bajeti, Bungeni jijini Dodoma.
Kwa Niaba ya Naibu Waziri wa Maji ,Wakili Nandule amesema lengo la kuanzishwa kwa Mfuko wa Taifa wa Maji ni kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali fedha ya uhakika katika kusaidia kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maji itakayoboresha huduma ya upatikanaji wa huduma ya maji nchini pamoja na kuimarisha usimamizi na uendelezaji wa vyanzo vya maji.

Mfuko wa Taifa wa Maji umekuwa ukitoa miongozo ya utoaji wa fedha katika utekelezaji wa miradi ya maji na ufuatiliaji wa fedha hizo.
Amesema mfuko unaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuongeza wigo wa mapato kupitia vyanzo mbalimbali pamoja na kujenga hoja ili kupata nyongeza ya kutoka katika tozo ya mafuta ya petroli na dizeli.

